Responsive image
Responsive image
Posted : June 30, 2017 (11 months ago) By TBC
Responsive image
Spika wa Bunge, Job Ndugai
Responsive image

Bunge limesoma kwa mara ya kwanza miswada mitatu inayohusu rasilimali za maliasili za nchi ukiwemo mswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2017, Muswada wa sheria ya mapitio na majadiliano kuhusu masharti hasi katika mikataba ya maliasili za nchi wa mwaka 2017, pamoja na Muswada wa sheria ya mamlaka ya nchi kuhusiana na umiliki wa maliasili wa mwaka 2017.

 

Akitoa maelezo kuhusu Miswada hiyo Spika wa Bunge Job Ndugai amesema ameunda kamati mbili zitakazojadili, kuchambua, kuandaa na kutoa taarifa zitakazo wasilishwa bungeni kwa ajili ya kupitisha miswada hiyo kwa manufaa ya Taifa.

 

 Aidha Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kutokana na umuhimu wa miswada hiyo kwa taiafa bunge limeongeza muda wa siku tatu za kazi kwa ajili  ya kuchambua na kujadili miswada hiyo kwa kina.

 

 

KHALID GANGANA

JUNI 30,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment