Responsive image
Responsive image
Posted : June 30, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Taifa Stars imetinga Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) baada ya kutoka sare ya kufungana goli moja kwa moja na Mauritius
Responsive image

Timu ya Taifa Stars itamenyana Afrika Kusini ambao ni wenyeji wa michuano ya COSOFA katika robo fainali ya michuano hiyo jumapili ya Julai tatu mwaka huu.

 

Taifa Stars imetinga Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA)  baada ya kutoka sare ya kufungana goli moja kwa moja na Mauritius na hivyo kumaliza wakiwa vinara wa kundi A kwa kufikisha alama 5.

 

Pongezi kwake winga Simon  Msuva aliyetokea benchi kipindi cha pili na kwenda kuifungia Taifa Stars bao la kusawazisha dakika ya 68 ya mchezo  baada ya Mauritius kutangulia kupata bao la kuongoza katika dakika ya 67.

 

 

OSCAR URASA

JUNI 30,2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies FashionTwila Kambangwa Mtumbi  |  9 months ago   |   July 01, 2017
"Mpo vizuri TBC"

Leave Your Comment