Responsive image
Responsive image
Posted : June 30, 2017 (8 months ago) By TBC
Responsive image
Kiungo wa Ujerumani Leon Goreztka akishangilia katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la mabara ambapo Ujerumani ilishinda mabao 4-1 na kutinga fainali ya michano hiyo
Responsive image

Ujerumani imetinga fainali ya michano ya kombe la mabara (FIFA CONFEDERATION CUP 2017) baada ya kuiadhibu bila huruma Mexico kwa kipigo cha magoli Manne kwa Moja katika mchezo wa nusu fainali.

 

Leon Goreztka amepachika magoli mawili katika kipindi cha kwanza kabla ya Timo Warner na Amin Younes kulizamisha kabisa jahazi la Mexico katika kipindi cha pili huku goli pekee la kufutia machozi kwa Mexico likifungwa na Marco Fabian.

 

Kwa matokeo hayo Ujerumani itamenyana na Chile katika fainali siku ya jumapili baada ya chile kuisukuma nje ya mashindano Ureno katika hatua ya nusu fainali kwa changamoto ya mikwaju ya penati Mitatu kwa Sifuri kufuatia sare ya bila kufungana katika muda wa dakika miamoja ishirini.

 

 

OSCAR URASA

JUNI 30,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment