Responsive image
Responsive image
Posted : June 29, 2017 (8 months ago) By TBC
Responsive image
Virusi katika mfumo wa Kompyuta
Responsive image

Shambulio la virusi katika mfumo wa mtandao wa mawasiliano ya kielekroniki limeripotiwa  kuathiri  baadhi ya shughuli za makampuni mbalimbali ndani na nje ya bara la Ulaya.

 

Akizungumzia hali hiyo, mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika wizara ya mambo ya ndani ya nchini Ukraine Artem Shevchenko, amesema hali hiyo ilianzia nchini humo hapo jana  na kusambaa katika mataifa mengine ambapo imeathiri shughuli za usafirishaji katika viwanja vya ndege, safari za meli, maduka makubwa  na baadhi ya taasisi za fedha.

 

Tayari shambulio hilo la mtandao wa mawasiliano ya kielekroniki na mifumo yake imezikumba nchi za India, Uingereza, Russia na Ufaransa ambapo Ukraine imeripotiwa kuathiriwa zaidi na shambulio hilo tangu nchi hiyo ilipoanza kutumia mfumo huo katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii na biashara.

 

Hata hiyo baadhi ya  wataalamu wanaendelea na juhudi za kutatua tatizo hilo ili kurejesha mfumo wa mawasiliano hayo katika hali ya kawaida.

 

 

RAMADHANI MPENDA

JUNI 28,2017

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment