Responsive image
Responsive image
Posted : June 28, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Kibiti, Lindi
Responsive image

Watu wawili wameuawa akiwemo Mwenyekiti wa kijiji cha Mangwi kilichopo kata ya Mchukwi wilaya ya Kibiti mkoani Pwani kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

 

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani,  Onesmo Lyanga amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo pia wauaji hao wamemjeruhi kwa risasi mtu mwingine mmoja.

 

Amewataja waliouawa kuwa ni mwenyekiti wa kijiji cha Mangwi, Maiko Nikolaus na Mtendaji wa kijiji hicho Shamte Makawa.

 

Kwa mujibu wa kamanda Lyanga kikosi cha polisi tayari kimekwenda katika kijiji hicho kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa tukio hilo.  

 


 

JOSEPH CHEWALE

JUNI 28,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment