Responsive image
Responsive image
Posted : June 26, 2017 (8 months ago) By TBC
Responsive image
Jengo lililowaka moto mjini London lililojengwa chini ya kiwango.
Responsive image

Hali ya wasiwasi imezidi kuongezeka nchini Uingereza, baada ya majengo 34 kubainika kuwa hayako katika viwango na yanauwezekano wa kuwaka moto kama lilivyowaka moto jengo moja mjini London na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 70.

 

Majengo hayo yamebainika kuwa yamejengwa kwa kutumia vifaa kama vile vya jengo lililowaka moto ambavyo vinashika moto kwa haraka na kuhatarisha usalama wa watu wanaokuwa ndani ya majengo hayo.

 

Wasiwasi wa watu hao unaongezeka zaidi kwa vile watu wote waliokufa katika tukio la moto mjini London walikuwa wamelala usingizi wakati moto kwenye ghorofa hilo refu ulipowaka.

 

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May aliamuru kufanyika kwa uchunguzi katika majengo mengine marefu ambayo ni makazi ya watu ili kubaini usalama wake.

 

 

NYAMBONA MASAMBA

JUNI 25,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment