Responsive image
Responsive image
Posted : June 26, 2017 (8 months ago) By TBC
Responsive image
Maandamano nchini Venezuela kupinga serikali ya nchi hiyo.
Responsive image

Mamia ya wananchi wa Venezuela kwa mara nyingine wamejitokeza katika mitaa mbalimbali ya nchi hiyo kupinga serikali ya nchi hiyo.

 

Maandamano ya sasa yameanzia katika eneo ambako mtu mmoja aliyekuwa akishiriki maandamano hayo alikufa, baada ya kupigwa risasi na polisi. Watu hao wamekasirishwa na kifo cha mtu huyo ambaye wanadai alikuwa akishiriki katika maandamano ya kudai haki.

 

Wapinzani nchini Venezuela wamekuwa wakihamasisha maandamano ya kupinga serikali ili kumshinikiza rais Nicolas Maduro wa nchi hiyo kuachia madaraka. Watu hao wanamuona Maduro kuwa chanzo cha mdororo wa uchumi nchini mwao.

 

 

NYAMBONA MASAMBA

JUNI 25,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment