Responsive image
Responsive image
Posted : June 23, 2017 (11 months ago) By TBC
Responsive image
Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Lucas Mkondya.
Responsive image

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM limesema litaimarisha ulinzi na usalama wakati wa Siku Kuu ya Idd El Fitr inayotarajiwa kuwa mwishoni mwa wiki au mapema wiki ijayo na kuonya watakaobainika kufanya uhalifu watachukuliwa hatua za kisheria.

 

Akizungumza jijini DSM, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Lucas Mkondya amesema doria za vikosi vyote ikiwemo vya farasi na mbwa zitaimarishwa huku akiwataka wananchi kusheherekea siku kuu hiyo kwa utulivu.

 

Kuhusu matukio ya uhalifu Kamanda Mkondya amesema jeshi hilo limekamata bunduki moja na bastola katika matukio mawili ya uhalifu Kigogo Luhanga na Mabibo Mpakani jijini DSM ambapo watu wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi wameuawa na mmoja kujeruhiwa katika mapambano na polisi kwenye matukio hayo.

 

 

DOMINIC MOKIWA

JUNI 23, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment