Responsive image
Responsive image
Posted : June 23, 2017 (8 months ago) By TBC
Responsive image
Qatar
Responsive image

Mataifa manne ya kiarabu yameitumia Qatar masharti 13 ambayo ni sharti iyafikie iwapo inataka kuondolewa vikwazo.

 

Taarifa mbalimbali za vyombo vya habari zinaarifu kuwa Saudia, Misri, Umoja wa Nchi za Kiarabu na Bahrain zinataka taifa hilo kufunga kituo chake cha habari cha Aljazeera. 


Aidha wanaitaka Qatar kupunguza ushirikiano na Iran na kufunga kambi moja ya wanajeshi ya Uturuki katika kipindi cha siku 10 pekee.


Taifa hilo limekabiliwa na vikwazo vya kidiplomasia na kiuchumi kwa kipindi cha wiki mbili ikiwa ni mgogoro mbaya zaidi wa kisiasa kati ya mataifa hayo ya Ghuba kwa miongo kadhaa.


Orodha hiyo ilitangazwa baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson kuwaambia majirani wa Qatar kuweka mahitaji yao na kuchukua hatua.

 

 

EDWARD KONDELA
JUNI 23, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment