Responsive image
Responsive image
Posted : June 19, 2017 (10 months ago) By TBC
Responsive image
Watuhumiwa wa uhujumu uchumi waliotajwa katika kashfa ya escrow mahakamani.
Responsive image

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa -TAKUKURU imewafikisha mahakamani mmiliki wa Kampuni ya Pan Afrika Power –PAP, Harbinder Sethi Singh na mfanyabiashara James Rugemalira kwa tuhuma za uhujumu uchumi.

 

Watuhumiwa hao wawili wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini DSM kwa tuhuma za uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara.Wakiwa kizimbani watuhumiwa  hao wote kwa pamoja wamesomewa mashtaka manne yakiwemo ya kula njama ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka Benki Kuu ya Tanzania - BOT pamoja na kujihusisha na mtandao wa uhalifu kwa kushirikiana na watumishi wa umma.Kwa upande wa James Rugemarila anakabiliwa na mashtaka Sita likiwemo la kughushi cheti cha usajili wa kampuni.

 

Watuhumiwa wamepelekwa rumande kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo  ambayo itatajwa tena JULAI 3 mwaka huu

 

 

VUMILIA MWASHA

JUNI 19,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment