Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi Ahmed Msangi.
Jeshi la polisi mkoani Mwanza linawashikilia wafanyabiashara wawili wakazi wa Kona ya Bwiru jijini Mwanza kwa tuhuma za kupatikana na shehena ya zana za uvuvi haramu zilizopigwa marufuku.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi Ahmed Msangi amesema operesheni dhidi ya wale wanaojihusisha na biashara zana haramu za uvuvi inaendelea ili kuhakikisha uvuvi haramu katika ziwa Victoria unatokomezwa.
REGINA NDESIKA
JUNI 19,2017