Responsive image
Responsive image
Posted : June 19, 2017 (9 months ago) By TBC
Responsive image
Mtu huyo alikufa papo hapo baada ya kugongwa na gari hilo ndani ya msikiti.
Responsive image

Baraza la waislamu nchini Uingereza limesema mtu mmoja amekufa na wengine kumi kujeruhiwa baada ya mtu mmoja kwa makusudi kuendesha gari lake na kwenda kuwagonga watu waliokuwa wakiswali msikitini mjini London.

Mtu huyo alikufa papo hapo baada ya kugongwa na gari hilo ndani ya msikiti. Polisi nchini Uingereza wamemkamata mtu mmoja mwenye umri wa miaka 48 aliyekuwa akiendesha gari hilo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kukusudia.

Polisi nchini Uingereza wamesema tukio hilo lina kila dalili ya kuwa la kigaidi na wameongeza ulinzi katika mji wote wa London.

 

 

Nyambona Masamba

Juni 19,2017

==

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment