Responsive image
Responsive image
Posted : June 19, 2017 (11 months ago) By TBC
Responsive image
Rais, Dkt. John Magufuli.
Responsive image

Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo la Kusini mwa Tanzania limesema kuwa linamuunga mkono Rais DKT.John Magufuli kwa kazi yake nzuri anayoifanya ya kuimarisha uchumi wa nchi na kuwafichua wahujumu uchumi.

 

Kauli hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Mark Malekana  wakati wa Ibada maalum ya kanisa hilo, ambapo pia kumefanyika uzinduzi wa Programu Mpya ya kuwafikishia injili Watanzania wote.

 

  Mkuu wa wilaya ya Rungwe Chalya Julius kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala, amesema serikali itaendelea kuimarisha amani ili waumini wote wa dini mbalimbali waendelee kuabudu kwa amani na utulivu.

 

 Aidha waumini hao pia wametoa huduma ya afya, ikiwa ni pamoja na kujitolea damu kwaajili ya kuongeza akiba ya damu nchini.

 

 

HOSEA CHEYO   

JUNI 19, 2017                  

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment