Responsive image
Responsive image
Posted : June 19, 2017 (11 months ago) By TBC
Responsive image
Maji.
Responsive image

Halmashauri ya wilaya ya Bunda Vijijini mkoani Mara imeelezea kuridhishwa na utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyang’aranga  unaotekelezwa na Serikali kupitia msaada kutoka benki ya Dunia na Shirika la Kimataifa la Misaada la Japan – JICA.

 

 Mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya Audacia  Investment Limited  ya kutoka Jijini  Dar es salaam utakapokamilika utaziwezesha kaya elfu saba katika Halmashauri hiyo kupata huduma ya maji safi na salama.

 

 Makamu Mwenyekiti Wa Halmashauri Ya Bunda Vijijini Sabato Mafwimbo amesema mradi huo unaendelea vizuri na utakapokamilika utakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi.

 

Ujenzi wa mradi huu mkubwa wa maji katika kijiji cha Nyang’aranga  umeanza kutekelezwa mwaka2015 na unatarajiwa kukamilika  juni 2017 kwa gharama ya zaidi ya shilingi  milioni 700.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment