Responsive image
Responsive image
Posted : June 06, 2017 (10 months ago) By TBC
Responsive image
Doha, Qatar.
Responsive image

Qatar imekanusha kuwasaidia wapiganaji wa makundi  mbalimbali  ikiwemo ya Islamic State na  Al Qaeda na kusema hatua ya mataifa matano kukataa uhusiano na nchi hiyo kwa madai ya kuyasaidia makundi ya wapiganaji  sio ya haki.

 

Mataifa matano ya kiarabu Saudi arabia, Misri, muungano wa falme za kiarabu( UAE), Bahrain na Yemen yalikataa mahusiano ya kidiplomasia na nchi ya Qatar kwa madai kuwa Qatar imekuwa ikiwasaidia wapiganaji wa makundi  mbalimbali  ikiwemo ya Islamic State na  Al qaeda na kusababisha ukosefu wa amani.

 

Uamuzi wa mataiafa hayo dhidi ya Qatar unafuatia kuvuja kwa baadhi ya barua pepe zinazoonyesha namna nchi hiyo ilivyokuwa ikiwasiliana na makundi ya Islamic state, kundi la udugu wa kiislamu pamoja na kudi la Al qaeda.

 

 

ANETH ANDREW

JUNE 06,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment