Responsive image
Responsive image
Posted : June 04, 2017 (11 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri mkuu wa Uingereza, Thereza May.
Responsive image

Waziri mkuu wa Uingereza, Thereza May amesema imetosha, au kwa lugha ya kingereza Enough Is Enough, kwa magaidi ambao wameendelea kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

 

Akihutubia taifa muda mfupi uliopita May amesema, wananchi wa Uingereza wakiungana kwa pamoja, bila kujali tofauti zao za kiitikadi na kidini, wanaweza kabisa kutokomeza vitendo vya ugaidi nchini humo.

 

Kiongozi huyo amesema, muda wa kuwavumilia magaidi wanaodharau thamani ya taifa umekwisha, kwani wameendelea kuhatarisha usalama wa wananchi wa Uingereza, na hivyo taifa hilo limeamua kutumia mbinu mpya za kukabiliana nao.

 

Amesema magaidi ambao wanakuja kwa mwamvuli wa dini ya kiislamu na kudharau ustaarabu wa nchi za magharibi kwa kisingizio cha dini wanapaswa kudhibitiwa katika mitandao yote wanayotumia kwa mawasiliano, pamoja na mataifa mengine.

 

May amesema maisha ya wananchi wa Uingereza yanapaswa kuendelea kama kawaida, licha ya watu wachache wanaotaka kuzusha hofu katika taifa hilo, hivyo kampeni za uchaguzi zinazoendelea nchini humo, zitaendelea tena kesho kama kawaida.

 

May amesema uchaguzi mkuu wa Uingereza uliopanga kufanyika siku ya Alhamisi wiki hii utafanyika kama ulivyopangwa.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment