Responsive image
Responsive image
Posted : June 04, 2017 (11 months ago) By TBC
Responsive image
Ofisi za Umoja wa Mataifa.
Responsive image

Umoja wa mataifa umetoa wito wa kuchukuliwa kwa watua za haraa ili kukomesha kile umoja huo uliokiita duru ya mashambulio nchini Afghanistan, baada ya watu ishirini kuuawa wakati wa mazishi mjini Kabul.

 

Mabomu matatu yaliyolipuka yaliwalenga waombolezaji waliokuwa wamehudhuria kwenye mazishi hayo ya mtoto na kaumu spika wa Afghanistan, Salim El Zadya aliyeuwa alipokuwa akishiriki katika maandamano ya kupinga serikali.

 

Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema, mara baada ya shambulio, vipande vya miili ya watu waliokuwa wamelipuliwa na mabomu hayo ilionekana ikiwa imesambaa makaburini. Hadi sasa hakuna kikundi chochote kilichodai kuhusika na mashambulio hilo.

 

Serikali ya Afghanistan inasema, inapenda kuwalinda raia wake dhidi ya mashambulio ya kigaidi nchini humo.

 

Wapiganaji wa kikundi cha TALEBAN cha nchini humo wanasema, hawapaswi kulaumiwa kwa shambulio la Jumamosi la kuigaidi au dhidi ya shambulio baya kuliko yote kuwahi kutokea nchini humo katika siku za hivi karibuni, lililoteka siku ya Ijumaa na kusababisha vifo vya watu TISINI.

 

Shambulio hilo lilitokea katika maeneo yenye balozi za kigeni nchini AFGHANISTAN.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies FashionMalimi Chenya  |  11 months ago   |   June 06, 2017
"Wapiganaji wa kikundi cha TALEBAN basi mumetosha acheni kuua raia wasio na hatia kwani ni dhambi kubwa sana kwa mungu,hao ni binadamu wenzenu acheni kabisa mungu hajaribiwi na mtu,sote ni ndugu moja."
Ladies Fashionmalimi chenya  |  10 months ago   |   June 09, 2017
"Acheni Kuua Raia Wasio Na Hatia"

Leave Your Comment