Responsive image
Responsive image
Posted : June 02, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Mwenge wa Uhuru.
Responsive image

Mwenge wa uhuru umenza mbio zake mkoani Pwani ambapo utatembelea miradi 81 yenye thamani ya shilingi bilioni 225.13.

 

Akipokea mwenge huo kutoka mkoani DSM Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist  Ndikilo, amesema ukiwa mkoani humo utakimbizwa katika halmashauri 9 na  kuzindua,  kuweka mawe ya msingi na kufungua miradi mbalimbali ambayo imetekelezwa kwa ushirikiano kati ya serikali, wananchi pamoja na wahisani wa maendeleo.

 

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa  Amour Hamad Amour amewaasa wananchi wa wilaya ya Mafia kutoa fursa sawa kwa watoto wa kiume na wakike kusoma ili kuandaa taifa lenye wataalamu wa kutosha.

 

Mwenge wa uhuru umeingia mkoani Pwani ukitokea mkoa wa Dar es salaam ambapo ulipitia miradi 40  yenye zaidi ya shilingi  bilioni 234.

 

 

JOSEPH CHEWALE

JUNE 02,2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment