Responsive image
Responsive image
Posted : May 24, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli akipokea taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini -Makinikia yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Responsive image

 

Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini itajazwa baadaye.

Awali rais Magufuli ameivunja Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania – TMAA na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa wakala huo, Mhandisi Dominic Rwekaza kutokana na mianya ya upotevu wa mapato ya mchanga wa madini.

Maamuzi hayo yamefanyika baada ya rais kupokea taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza mchanga ulio katika makontena ya mchanga wa madini -Makinikia yaliyopo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Rais Magufuli anasubiri ripoti ya kamati ya pili iliyopewa jukumu la kuangalia athari za uchumi na kisheria zilizotokea kipindi chote ambapo mchanga huo ulikuwa ukisafirishwa kwenda nje ya nchi.

Kamati hizo mbili ziliundwa na Rais Magufuli baada ya mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu kufanya ziara ya kushtukiza bandari ya DSM na kubaini makontena ya mchanga wa dhahabu yakisafirishwa nje ya nchi na kutilia shaka uhalali wa ukaguzi wake na kuziagiza kufanya uchunguzi.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies FashionEDWIN H MATHIAS  |  12 months ago   |   May 26, 2017
"Nampongeza mheshimiwa Rais kwasababu tuliibiwa mno"

Leave Your Comment