Responsive image
Responsive image
Posted : May 20, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Yanga mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara 2017
Responsive image

Licha  Yanga kufungwa bao moja kwa bila na Mbao Fc katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba,timu hiyo imekabidhiwa kombe la  ubingwa wa michuano hiyo baada kufikisha alama 68 sawa na watani wao wa Jadi Simba,lakini wanawastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Timu ziloshuka daraja kuungana na Ruvu JKT,ni African Lyon ambayo ametoka suluhu na Tanzania Prisons, ,Toto Africans ambayo imefungwa na mitibwa mabao matau kwa moja.

Matokeo ya michezo mingine,majimaji imeifunga mbeya city mabao mawili kwa moja wakati ,azam fc ikilala kwa bao moja kwa bila dhidi ya Kagera Sugar,huku simba ikibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Mwadui Fc ya shinyanga na Stand United imeifunga Ruvu Shooting bao moja kwa bila.

Simba imengomea kuchukua zawadi ya mshindi wa pili hadi rufaa yao itakaposikilizwa na FIFA, simba imekata rufaa FIFA, kupinga,kupokwa pointi tatu na shirikisho la soka nchini TFF na kurejeshewa Kagera Sugar  ambayo inadaiwa kumchezesha beki wake Mohmed Fakhi ambaye anadiwa alikua na kadi tatu za njano.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment