Responsive image
Responsive image
Posted : March 22, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Wachezaji wa Taifa Stars Mazoezini
Responsive image

Wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa stars) wamepimwa utimamu wa mwili kabla ya kuanza  mazoezi ya kuivaa timu ya taifa ya Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa siku ya  Jumamosi kwenye dimba la Taifa.

 

Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema,wachezaji Mbwama Samatta na Faridi Mussa wamekosa vipimo hivyo lakini watafanyiwa vipimo hivyo watapowasili hapa nchini.

 

Katika hatua nyingine TFF imekanusha kuwa hakuna mpango wowote wa Taifa stars kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Zambia kwasababu chama cha soka cha Zambia (FAZ) hakikujibu mapema maombi ya TFF ya kucheza mchezo huo wa kirafiki.

 

Stars itacheza mechi mbili za kirafiki za kujipima nguvu dhidi ya Botswana na Burundi chini ya kocha mpya Salum Mayanga aliechukua mikoba hiyo toka kwa Charles Bonifance Mkwasa ambae hivi sasa ni katibu mkuu wa timu ya Yanga.

 

 

CHETO NJEDENGWA

MACHI 21, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment