Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Emirates itapunguza safari za ndege kwenda Fort Lauderdale, Orlando, Seattle, Boston na Los Angeles
Responsive image

 

Shirika la Ndege la Emirates limetangaza kwamba litapunguza safari za ndege zake hadi Miji Mitano ya marekani kuanzia mwezi ujao.

Hatua hiyo inatokana na marufuku iliyowekwa na Serikali ya Rais Donald Trump kuzuia baadhi ya raia wa mataifa yenye Waislamu wengi kuingia Marekani pamoja na masharti mengine makali ya kiusalama.

Emirates imesema mabadiliko hayo yanatokana na kushuka kwa idadi ya watu wanaosafiri kwenda Marekani.

Mwezi uliopita Marekani ilipiga marufuku vifaa vya kielektroniki ambavyo ni vikubwa kuliko simu kwenye sehemu ya mizigo ya ndege kutoka viwanja 10 vya ndege.

Viwanja hivyo ni pamoja na vya Dubai, na mataifa mengine ya Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini na Uturuki.

Emirates imesema itapunguza safari za ndege kwenda Fort Lauderdale, Orlando, Seattle, Boston na Los Angeles

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment