Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Wapinzani wawili walioungana ili kumng'oa Mugabe
Responsive image

Wapinzani wawili wakuu wa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe wameungana ili kuhakikisha kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 anaondoka madarakani.

Wapinzani hao Morgan Tsvangirai Kiongozi wa Chama cha Movement for Democratic Change -MDC na Joice Mujuru ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Mugabe hadi alipofukuzwa mwaka 2014 wamesema watapigania kuunda serikali ya mseto ili kuleta mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Chama Tawala nchini Zimbabwe ambacho kinaiongoza nchi hiyo tangu ipate uhuru wake mwaka 1980 Desemba mwaka jana kilimpitisha rasmi Rais Mugabe kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika katikakati ya mwaka ujao ambapo kiongozi huyo atakuwa ametimiza umri wa miaka 94.

Wapinzani wanamlaumu Rais Mugabe kwa kuua uchumi wa Zimbabwe ambayo ni moja ya nchi za Kiafrika iliyokuwa na ustawi mkubwa.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI
Ladies FashionLois  |  6 months ago   |   December 07, 2017
"Appreciate this post. Will try it out. maglia lazio bambini"

Leave Your Comment