Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
Responsive image

 

Rais  Dkt. John Pombe Magufuli ametoa ajira kwa Madaktari 258 na wataalamu wengine wa afya 11 waliokuwa wamekidhi vigezo vya kwenda kufanya kazi nchini Kenya kwa mkataba.

Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema hatua hiyo imekuja baada ya Madaktari watano wa Kenya kuweka pingamizi mahakamani na kuitaka serikali ya nchi yao kusitisha kuajiri madaktari kutoka Tanzania.

 

 

BERTHA MWAMBELA

APRILI 19, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment