Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Bodi ya utalii nchini TTB itatumia vyombo vya habari vya Israeli kutangaza vivutio vilivyopo hapa nchini
Responsive image

Bodi ya utalii nchini TTB imeanza kutangaza vivutio vya utalii  nchini  Israeli kwa lengo la kupata watalii wengi kutoka ukanda wa mashariki ya kati.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa TTB jaji mstaafu Thomas Mihayo amesema bodi hiyo imeamua kutafuta soko la utalii nchini Israeli kutokana na kuanza kuimarika kwa uhusiano baina ya tanzania na Israel .

Kwa upande wake mkurugenzi wa bodi ya utalii Devota Mdachi amesema bodi itatumia  vyombo vya habari vya Israeli kutangaza vivutio vilivyopo hapa nchini pamoja na kuanzisha ushirikiano na bodi ya utalii ya nchi hiyo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment