Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
mashabiki wa timu ya simba
Responsive image

Ikiwa bado sakata la klabu ya Simba kupewa alama ilizopokwa timu ya Kagera Sugar bado halijapatiwa ufumbuzi, Uongozi wa klabu ya Simba umelijia juu na kulitaka shirikisho la soka nchini, TFF, kuitendea haki timu hiyo.

Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara, amesema utaratibu unaoendelea hivi sasa ambapo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kusikiliza shauri la Kagera Sugar ni kinyume na matakwa ya timu Kagera Sugar ambayo iliomba kupitiwa upya kwa uamuzi wa kesi iliyopelekea wao kupokwa alama tatu

Kamati ya saa 72 ya Ligi Kuu Tanzania Bara, iliipoka alama tatu timu ya Kagera Sugar na kupewa Simba baada ya kubainika imemchezesha mchezaji Mohamed Fakhi aliyekuwa na kadi tatu za njano kwenye mchezo wake dhidi ya Simba.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment