Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Mchezaji Tennis mwanadada, Petra Kvitova
Responsive image

Mchezaji Tennis mwanadada, Petra Kvitova amesema anaweza kuwashangaza watu pale ataporejea uwanjani hivi karibu na kushiriki mashindano ya wazi ya Ufaransa (France Open) mwezi ujao.

Nyota huyo kwa sasa anauuguza majeraha ya mkono aliyoyapata baada ya kushambuliwa na waharifu nyumbani kwao nchini Czech mwezi Desemba mwaka jana.

Petra Kvitova amesema anaendelea vizuri mno na anajionio anaweza kushiriki mashindano hayo makubwa ya Tennis ingawa alitakiwa kukaa njee ya uwanja kwa kipindi cha miezi sita.

Pamoja na kusema hivyo ila hana hakika sana kama atacheza mashindano hayo ila kwa sasa anajiweka sawa kisaikologia kuwa anaweza kushiriki mashindano hayo makubwa ya Tenis ambayo yataanza kutimua vumbi mei 28.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment