Responsive image
Responsive image
Posted : April 19, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
maeneo yaliyozingirwa na vita nchini Syria
Responsive image

Zoezi la kuwaondoa watu kutoka katika maeneo yaliyozingirwa na vita nchini Syria limeanza tena leo siku kadhaa baada shambulio la kujitoa muhanga kushambulia msafara wa magari na kusababisha vifo.

Zoezi hilo ni sehemu ya makubaliano hayo yaliyofikiwa na waasi na Serikali ya Syria.

Kiasi ya mabasi 45 yaliyowachukua watu 3,000 yaliondoka katika Miji ya Foua na Kefraya karibu na Mji wa Idlib kwenda katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali.

Msafara mwingine wa mabasi 11 umeondoka katika eneo linalodhibitiwa na Jeshi la Serikali la Zabadani.

Siku ya Jumamosi shambulio la bomu dhidi ya msafara huo kutoka Foua na Kefraya ulisababisha vifo vya watu 126 ikiwa ni pamoja na zaidi ya watoto 60.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment