Responsive image
Responsive image
Posted : April 19, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
mamia ya wananchi wa Ethiopia wakiandamana kupinga serikali ya nchi hiyo
Responsive image

 Serikali ya Ethiopia imekataa uchunguzi unaotaka kufanywa na Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa ulaya kuhusu  vifo vya mamia ya watu wakati wa maandamano ya kupinga serikali.

 Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn amesema nchi yake inauwezo wa kufanya uchunguzi yenyewe.

 Waandamanaji katika majimbo ya  Amhara na Oromia wameendelea kupinga kitendo cha kutengwa  kisiasa na kiuchumi.

Tayari serikali ya Ethiopia imetangaza hali ya hatari kutokana na maandamano hayo ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara tangu mwaka 2015.

 Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameripoti kuuawawa kwa mamia ya watu wakati wa mapambano kati yao na polisi

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment