Responsive image
Responsive image
Posted : April 19, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka na kauli mbiu ya wilaya moja bidhaa moja
Responsive image

 

 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka ametangaza mkakati maalumu  wa mkoa huo wenye kauli mbiu ya wilaya moja bidhaa moja ambao una maana ya kwamba kila wilaya katika mkoa huo inazalisha bidhaa moja kubwa ikiwa nisehemu ya utekelezaji wa malengo ya serikali ya awamu ya tano ya kufikia   tanzania ya viwanda ili kukuza uchumi na kuongeza wigo mpana wa  ajira kwa vijana .  

Akizungumza wakati wa mkutano wa wajumbe wa kitaifa wa shirikisho la wanataaluma na wajasiriamali  waadventista wasabato Tanzania Mtaka amesema  mkakati huo  unalenga kuongeza uzalishaji wa bidhaa za viwandani  ambao utapunguza kwa  asilimia 40 uingizaji wa bidhaa  kutoka nje ya mkoa huo.

Aidha Mtaka amesema serikali mkoani Simiyu imeanza mkakati wa ujenzi wa kiwanda cha  kuzalisha bidhaa zinazotokana na zao la pamba,kwa ajili ya matumizi ya mbalimbali ya hospitali hapa nchini

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment