Kundi la pili la wachezaji wa Yanga lilokuwa limechelewa ndenge nchini Algeria limewasali Jijini Dar es salaam
Kundi la pili la wachezaji wa Yanga lilokuwa limechelewa ndenge nchini Algeria limewasali Jijini Dar es salaam na baadhi yao kuwakimbia waandishi wa habari waliofika kwa ajili ya mahojiano.
Wachezaji hao wamewasili saa tisa na nusu wakiwa kumi na moja na jambo lililoshangaza wengi ni pale walipoamua kuwakimbia waandishi wa habari.
Gari la Yanga lilofika uwanja wa ndege kuwachukua wachezaji hao lilijikuta likiondoka na wachezaji wawili Beno Kakolanya na Emenuel Martin pamoja na katibu kuu wa Yanga Charles Mkwasa huku wengine wakitimbea kuelekea kituoni na wengine wakipanda magari binafsi.
Yanga imetolewa katika michuano ya kombe la shirikisho na timu ya Alger ya Algeria kwa jumala ya magoli manne kwa moja.