Responsive image
Responsive image
Posted : April 19, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Waziri Mkuu wa Somalia, Hassan Ali Khayre
Responsive image

Nchi ya Somalia imeomba mechi zake za kimataifa za timu yake ya Taifa zichezwe ndani ya nchi hiyo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo mechi zake zimekuwa zikichezwa nchi jirani ya Djibouti.

Ombi hilo limetolewa na waziri Mkuu wa Somalia, Hassan Ali Khayre kwa Rais wa CAF, Ahmad ambae yupo ziarani nchi humo tangu jana Jumatatu ambapo amesema serikali ya nchi hiyo ipo tayari kutoa ulinzi wa kutosha ili kuhakikisha michezo ya kimataifa inachezeka na kuna kuwepo na amani wakati wa mchezo.

Waziri huyo mkuu amemuomba Rais huyo wa CAF kuweza kulifanikisha jambo hilo kwa sababu wananchi wa Somalia wanataka kuiona timu yao ya Taifa (The Ocean Stars) ikicheza kwenye ardhi ya nyumbani na kuishangilia kama wanavyofanya watu wengine wa mataifa mbalimbali kwa timu zao za Taifa pamoja na kuona timu zingine za Taifa zikipambana na timu yao ya Taifa ndani ya Somalia sio kwenye nchi jirani ya Djibouti.

Kwa upande wake Rais wa CAF, Ahmad alimshukuru Waziri Mkuu huyo wa Somalia na kumuahidi kuwa CAF itafanya kila linalowezekana kusaidia kuwepo kwa amani nchini Somalia kupitia mchezo wa soka kwasababu soka ni mchezo wa mshikamano na unaleta watu pamoja.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment