Responsive image
Responsive image
Posted : April 18, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Baadhi ya wananchi wa Sri-Lanka wakifuatilia zoezi la uokoaji kwa majonzi
Responsive image

Zoezi la kuwatafuta watu ambao hawajulikani walipo baada ya nyumba zao kuangukiwa na dambo katika eneo la Meetotamulla, mjini Colombo, nchini Sri-Lanka linaendelea.

Waokoaji wanasema watu ishirini na wanane wamethibitika kufa baada ya moto mkubwa kuteketeza dampo hilo na kisha mvua kubwa kunyesha.

Hali hiyo imesababisha mlima wa taka uliokuwa kwenye dampo hilo, kulainika na kuangukia makazi ya watu wanaoishi karibu na eneo hilo.

Waokoaji wanasema zoezi la kuwaokoa watu hao linakwenda polepole kutokana na uhaba wa vifaa na hukofia kuwajeruhi watu waliofukiwa na kifusi cha taka au kuharibu miili ya watu waliofukiwa.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment