Responsive image
Responsive image
Posted : April 18, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Wafungwa elfu moja kutoka katika Mamlaka ya Palestina washikiliwa katika magereza mbalimbali nchini Israel
Responsive image

Wafungwa elfu moja kutoka katika Mamlaka ya Palestina wanaoshikiliwa katika magereza mbalimbali nchini Israel, wameanza mgomo wa kula chakula, ikiwa ni hatua ya kupinga serikali ya Israel kuwashikilia kwenye magereza hayo.

Watu hao wanaishutumu serikali ya Israel kwa kushiriki katika vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya wafungwa na watu wanaoshikiliwa katika magereza ya nchi hiyo, hususani kutoka katika Mamlaka ya Palestina.

Wakati huo huo, Mamia ya vijana wa Kipalestina wamewashambulia kwa mawe askari wa Israel, wakipinga vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu wanaofanyiwa wapalestina katika magereza ya Israel.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment