Responsive image
Responsive image
Posted : April 18, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Kocha wa timu ya Chelsea, Antonio Conte
Responsive image

Kocha wa timu ya Chelsea, Antonio Conte amesema yeye ndie anaepaswa kulaumiwa kwa timu yake kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Manchester United.

Kocha huyo muitaliano amekiri kuwa timu yake haikucheza mchezo mzuri na Manchester United walistahili kushinda na kwamba yeye kama kocha alishindwa kuwahamasisha wachezaji wake wapambane kupata ushindi.

Jana Manchester United iliifunga Chelsea bao mbili kwa bila kwa magoli yaliyofungwa kila kipindi na chipukizi Marcus Rashford na Ander Herrera huku Chelsea wakizidiwa kwenye kila idara na kushindwa hata kupiga shuti moja lilolenga lango kwa dakika zote 90.

Kwa matokeo hayo Chelsea inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi nne tu na timu inayoifuatia ambayo ni Tottenham Spurs na Conte akasema timu hiyo ya Kaskazini mwa London inaleta upinzani mkubwa wa kikosi chake kwasababu hivi sasa iko kwenye kiwango kizuri na wanapambana kweli kweli kitu ambacho wachezaji wake inabidi wafanye.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment