Responsive image
Responsive image
Posted : April 16, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, PAPA FRANCIS katika misa ya Pasaka kwenye Kanisa la Basilica huko Vatican Mjini Roma, Italia.
Responsive image

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani PAPA FRANCIS amewataka waumini wa Kiristo pamoja na jamii kuadhimisha Siku Kuu ya Pasaka kwa kuwajali watu wenye uhitaji hasa makundi ya watu wanaokabiliwa na ukatili na mateso.

 

Akizungumza katika misa kwenye Kanisa la Basilica huko Vatican Mjini Roma, Italia Papa Francis amesema baadhi ya watu wanakabiliwa na mateso hasa wale masikini wanaoomba misaada kwenye miji mbalimbali duniani pamoja na wale wanaoathirika na biashara haramu ya usafirishaji binadamu.

 

Amesema jamii inapaswa kuwajali watu hao wamepoteza dira na ndoto za maisha yao kutokana na vitendo vya unyonyaji, ukandamizwaji na ukatili.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment