Responsive image
Responsive image
Posted : April 16, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Gavana wa zamani wa Jimbo la Veracruz nchini Mexico chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa kwa tuhuma za ulaji rushwa, ubadhirifu wa mamilioni ya fedha pamoja na kujihusisha na vitendo vingine vya uhalifu.
Responsive image

Polisi nchini Mexico wamemkamata Gavana wa zamani wa Jimbo la Veracruz kwa tuhuma za ulaji rushwa, ubadhirifu wa mamilioni ya fedha pamoja na kujihusisha na vitendo vingine vya uhalifu.

 

Polisi wamesema Javier Duarte ambaye amekamatiwa katika Mji wa Solala nchini Guatemala amekuwa akitafutwa tangu mwaka 2016 nchini MEXICO huku akiwakwepa polisi.

 

Kukamatwa kwa Javier Duarte kumewezeshwa kwa msaada wa polisi wa Guatemala na wale wa Kitengo cha Polisi wa Kimataifa - Interpol.

 

Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mexico amesema mtuhumiwa huyo anatarajiwa kurejeshwa nchini humo ili ajibu mashitaka yanayomkabili.

 

Javier Duarte anatuhumiwa kujipatia Dola Milioni 28 za Kimarekani kwa njia za udanganyifu.

 

Pia anakabiliwa na tuhuma za mauaji ya waandishi wa habari 17 ambao waliuawa wakati wa utawala wake katika Jimbo la Veracruz.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment