Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Dodoma –TAKUKURU imebaini kuwepo kwa viashiria vya rushwa katika mabaraza ya usuluhishi na miradi ya maji katika baadhi ya wilaya mkoani humo.
Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma, Emma Kuhanga amesema hayo wakati akitoa taarifa ya utendaji wa mkoa kwa kipindi cha miezi Nane mwaka huu.
Kuhanga amesema utafiti huo umebaini viashiria vya rushwa hasa katika taasisi mbali mbali kuanzia ngazi ya kata ambapo tatizo la rushwa katika mabaraza ya usuluhishi ya kata limeshika kasi.
Aidha taarifa hiyo imeonyesha idara na taasisi zinazoongoza kuripotiwa juu ya tuhuma za vitendo vya rushwa ni TAMISEMI, taasisi za watu binafsi na polisi.
SHABANI KWAKA
APRIL 13