Responsive image
Responsive image
Posted : April 12, 2017 (12 months ago) By TBC
Responsive image
Gavana wa benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu
Responsive image

Matumizi ya simu za mkononi kwa ajili ya kutoa huduma za kifedha kumewezesha huduma za kifedha kuwafikia wananchi wengi kwa ukaribu  hasa wa vijijini na kuwawezesha kutuma na kupokea fedha

Hayo yamebainika  kwenye ripoti ya tisa ya hali ya uchumi wa Tanzania iliyotolewa na bank ya dunia  Jijini Dar es salaam ambapo  Gavana wa benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu amesema watanzania wanaotumia huduma za kifedha kwa sasa ni asilimia 60 kutoka asilimia 11 ya mwaka 2007 kutokana na kupata fedha kwa njia ya simu za mkononi

Kuhusu hali ya uchumi nchini ripoti hiyo imeonesha kuwa uchumi wa tanzania unaendelea kukuwa kwa asilimia saba ambapo unafanya vizuri ukilinganiasha na nchi nyingine za ukanda wa jangwa la sahara- ambapo Naibu waziri wa fedha na uchumi Dkt. Ashatu Kijaji amesema hali hiyo inachangiwa na serikali kupeleka fedha nyingi kwenye miradi ya maendeleo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment