Responsive image
Responsive image
Posted : April 06, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Kamishna mpya wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Bw.George Sakware akizungumza katika hafla ya kumuaga kamishna mstaafu wa TIRA Israel Kamuzora. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Bima la Taifa Bw. Sam Kamanga na kulia ni Kamishna Mstaafu Bw. Israel Kamuzora.
Responsive image

Kamishna mpya wa mamlaka ya usimamizi wa bima nchini TIRA Dkt.  George Sakware amezitaka kampuni za bima nchini kubuni huduma zitakazowafanya wananchi wa kipato cha chini kuvutiwa na kupanua wigo wa kuwafikia watu wengi zaidi.

 

Akizungumza na maafisa watendaji wa makampuni ya bima nchini wakati wa hafla ya kumuaga kamishna mstaafu wa TIRA Israel Kamuzora, Sakware amesema kumekuwa na changamoto ya kukua kwa sekta ya bima kutokana na kampuni kuwa na bidhaa zinazofanana na kuwalenga watu wa kipato cha juu.

 

Aidha mwakilishi wa umoja wa kampuni za bima nchini ambaye pia ni afisa mtendaji mkuu wa Kampuni ya Bima ya Jubilee George Alonde amesema kodi ya ongezeko la thamani inayotozwa katika ya bima inawakwaza wateja wao na wamelalamikia gharama za bima kupanda

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment