Responsive image
Responsive image
Posted : April 04, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo
Responsive image

Jumla ya shilingi trilioni 10.87 za kodi zimekusanywa na mamlaka ya mapato nchini TRA kwa kipindi cha miezi tisa cha mwaka wa fedha 2016 /2017  sawa na ukuaji wa asilimia 9.99 ukilinganisha na kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha 2015/2016

 

Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi wa TRA Richard Kayombo amesema makusanyo hayo ni ya kuanzia mwezi july 2016 mpaka march 2017 ambapo kwa mwezi Machi 2017  mamlaka hiyo ilikusanya shilingi trilioni 1.34.

 

Kayombo amesema TRA imeweka lengo la kukusanya shilingi tirioni 15.1 katika mwaka wa fedha 2016/2017 na lengo hilo litafikiwa kutokana na makusanyo ya kodi za majengo.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment