Responsive image
Responsive image
Posted : April 01, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe na Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Ethiopia Dkt. Hirut Teketel wakisaini mkataba wa makubaliano yanayotoa fursa za uwekezaji pamoja na mafunzo kwa wadau wa sekta ya utalii Ikulu Jijini Dar es salaam.
Responsive image

anzania na shirikisho la jamhuri ya kidemokrasia ya Ethiopia zimetiliana saini mikataba mitatu ya kuimarisha ushirikiano, kuanzisha kamisheni ya pamoja ya kudumu na hati ya makubaliano katika sekta ya utalii.

 

Utiaji saini huo umefanyika  Jijini DSM baina ya mawaziri wa Mambo ya Nje pamoja na Mawaziri wa Utalii wa nchi zote mbili.

 

Utiaji saini huo umeshughudiwa na viongozi mbalimbali wa serikali hizo wakiongozwa na Rais  John Magufuli na Waziri Mkuu wa shirikisho la jamhuri ya kidemokrasia ya Ethiopia Hailemariam Desaleign.

 

Baada ya zoezi hilo viongozi wakuu wa mataifa hayo mawili wakazungumza na hadhira ambapo Rais Magufuli amesema pamoja na mambo mengine, Waziri Mkuu wa shirikisho la jamhuri ya kidemokrasia ya Ethiopia amekubali kuanzishwa ushirikiano kati ya Shirika la Ndege la Ethiopia na Tanzania pamoja na kuagiza wataalam wa mabwawa makubwa ya umeme kufika Tanzania kuona jinsi ya kutekelezwa kwa miradi hiyo.

 

Nae Waziri Mkuu wa Ethiopia Haile Mariam DESALEIGN amesema nchi hizi mbili zina uhusiano wa kihistoria hivyo kuendelea kushirikiana ikiwa ni pamoja na shirikisho la jamhuri ya kidemokrasia ya Ethiopia kujifunza masuala ya kilimo Tanzania ni vipaumbele anavyoamini vitaimarisha ushirikiano wa nchi hizi mbili.

 

 

ELISHA ELIA

MACHI 31, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment