Responsive image
Responsive image
Posted : April 01, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJKNUAT), Profesa Dominic Kambarage
Responsive image

Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius K. Nyerere cha Kilimo na Teknolojia (MJKNUAT) kimejipanga kuanza kutoa mafunzo ya vitendo ya kilimo bishara kwa vijana kupitia mitaala maalum.

 

 Makamu Mkuu wa Cho hicho, Profesa Dominic Kambarage amesema lengo ni kukuza uchumi na kusaidia kupambana na tatizo la ajira hapa nchini.

 

Profesa Kambarage ametoa kauli hiyo wakati wa kongamono lililozikutanisha taasisi za kifedha, mifuko ya serikali na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC, kufikiria njia za kuwawezesha vijana kukipenda kilimo na kuingia katika kilimo cha biashara.

 

Kwa upande wake Afisa Mwandamizi, Ushawishi na Mawasiliano kwa Umma wa NEEC, Edward Kessy  amesema wanaunga mkono juhudi za chuo hicho katika kutoa mafunzo maalumu kwa vijana yatakayosaidia kuingia kwenye kilimo cha biashara.

 

 

 

VUMILIA MWASHA

MACHI 31, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment