Responsive image
Responsive image
Posted : March 31, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akiwa na Msanii Nay wa Mitego walipokutana katika ofisi za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mjini Dodoma na kuzungumzia maudhui ya wimbo wa msanii huyo uliofungiwa na kisha kuruhusiwa na Serikali hivi karibuni.
Responsive image

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema Tanzania ni nchi inayoheshimu Utawala wa Sheria na kuwataka Wasanii kutambua kuwa kazi yao ina umuhimu wa kipekee katika Jamii.

 

Dr Mwakyembe amesema hayo mbele ya mkutano na Waandishi wa Habari mjini Dodoma wakati alipokutana na Msanii Emmanuel Elibariki Munissi maarufu kama Ney wa Mitego kuzungumzia maudhui ya wimbo WAPO, ambao umekuwa gumzo kote mitaani.

 

Akizungumza juu ya umuhimu wa Sanaa kwa Jamii, Dr Mwakyembe amesema Wasanii, kama moja ya Kioo cha Jamii wana umuhimu wa kipekee katika kutafsiri Utaifa.

 

Kwa upande wake, Msanii Ney wa Mitego anawaasa Wasanii wenzake kushikamana na kuwa kitu kimoja ili kuifanya kazi yao iweze kuheshimika na wote.

 

 

IDD MAALIM

MACHI 31, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment