Responsive image
Responsive image
Posted : March 30, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Barua inayoanzisha mchakato wa UINGEREZA kujitoa kwenye umoja wa EU. Mchakato huo unatarajiwa kuchukua muda wa miaka miwili.
Responsive image

Nchi ishirini na SABA zinazounda Umoja wa nchi za ULAYA zimesema, hatua ya UINGEREZA kuanza kujitoa kwenye umoja huo inaweza kuridhiwa na kila nchi, baada ya maelezo ya kwanza kukubaliwa.

 

Kumekuwa na hali ya huzuni kwa mataifa yanayounda Umoja huo, baada ya jana UINGEREZA kuwasilisha rasmi waraka wenye maelezo ya kuanza kutekeleza kifungu namba hamsini cha Umoja huo cha kuanza kujitoa, baada ya wananchi kufanya maamuzi.

 

Kila nchi inaangalia kwa makini jinsi ambavyo inaweza kuachana na UINGEREZA.

 

Kwa upande wake UINGEREZA imesema, itaanisha hatua itakazochukua wakati injitoa kwenye umoja huo.

 

Zoezi la UINGEREZA kujitoa kwenye Umoja huo linatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka miwili, wakati baadhi ya nchi za Umoja wa ULAYA zikiwa na uwezo wa kupiga kura ya turufu kuizuia nchi hiyo kujitoa.

 

 

MACHI 30, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment