Responsive image
Responsive image
Posted : March 29, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa mambo ya nje wa India, Sushma Swaraj.
Responsive image

Waziri wa mambo ya nje wa India Sushma Swaraj  ameomba kufanyika kwa uchunguzi kufuatia tuhuma za kushambuliwa kwa Waafrika katika jimbo la Uttar Pradesh.

 

Msichana raia wa Nigeria anaarifiwa kutekwa na Waafrika wengine kushambuliwa hapo jana wakati wa maandamano ya kupinga kifo cha mtu mmoja raia wa India katika mji wa Noida yaliyokumbwa na ghasia.

 

Inahofiwa mtu huyo alipewa madawa ya kulevya kupita kiasi.

 

Raia kutoka Nigeria wanatuhumiwa kwa uuzaji madawa hayo, ambapo watano walikamatwa kuhusiana na kisa hicho lakini wakaachiliwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi.

 

Swaraj  amesema waziri mkuu wa jimbo la Uttar Pradesh amemhakikishia kwamba uchunguzi huru utafanywa kuhusu kushambuliwa kwa wanafunzi hao.

 

Kwa mujibu wa vyombo vya habari India watu watano wanashikiliwa na polisi kutokana na tukio hilo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment