Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, MWIGULU NCHEMBA.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba anatarajia kuwa mgeni rasmi katika tamasha la pasaka lilopangwa kufanyika April 16 mwaka huu uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.
Mwandaaji wa Tamasha hilo Alex Msama amesema Waziri Mwigulu Nchemba atakuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Wasanii mbalimbali kutoka ndani ya Tanzania na nje ya mipaka ya nchi watashiriki tamasha hilo ambapo tayari wasanii kutoka Kenya baadhi yao wamethibitisha kushiriki tamasha hilo.
Tamasha hilo pia litafanyika katika mikoa ya Dodoma, Mwanza ,Iringa pamoja na Mbeya