Responsive image
Responsive image
Posted : March 27, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Kikosi cha timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Tanzania, Serengeti Boys
Responsive image

Timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 ya Tanzania Serengeti Boys,watacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa ya kujipima nguvu dhidi ya vijana ya Ghana Aprili Pili mwaka huu kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam

 

Afisa Habari wa shirikisho la soka nchini TFF, Alfred Lucas ameimbia TBC jijini Dar es salaam kwamba mechi hiyo dhidi ya Ghana,itawaongezea uzoefu wachezaji wa Serengeti Boys kabla ya fainali za Afrika za vijana zitakazofanyika May nchini Gabon.

 

Tayari Serengeti Boys wapo Bukoba na wanatarajia kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Burundi,baada ya timu za taifa za Rwanda na Uganda kushindwa kucheza na timu hizo.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment