Responsive image
Responsive image
Posted : March 26, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars wakishangilia moja ya goli dhidi ya Timu ya Taifa ya Botswana
Responsive image

Timu ya Taifa ya Tanzania-Taifa Stars imepata ushindi wa magoli mawili kwa bila  dhidi ya Botswana  katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

 

Katika mchezo huo mashabiki wengi walijitokeza kuishangilia Taifa Stars wakiongozwa na waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Dkt.  Harisson Mwakyembe ambapo mmoja kati ya mashabiki aliyekuwa kivutio uwanjani hapo ni shabiki mlemavu wa macho ambaye pamoja na ulemavu huo hakuwa nyuma kuisangilia Taifa Stars.

 

Shabiki huyo Ally Musa maarufu Babually anasema kupenda kwake mpira wa miguu na mahaba yake kwa timu ya Taifa ndio kichocheo kikubwa kwake kujitokeza uwanjani na kuishangilia kwa nguvu timu ya taifa huku nahodha Mbwana Samatta akimpongeza shabiki huyo kwa uzalendo wake.

 

Magoli yote ya Taifa Stars yalifungwa na nahodha Mbwana Samatta.

 

 

EVANCE MHANDO

MACHI 25, 2017

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment