Responsive image
Responsive image
Posted : March 24, 2017 (one year ago) By TBC
Responsive image
Mh. Haji Mponda, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali akizungumza na Mama Blandina Nyoni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC
Responsive image

Kamati ya bunge ya hesabu za serikali imeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa nyumba za shirika la nyumba la taifa NHC inayotoa hifadhi kwa wananchi, biashara na kulipa kodi kwa serikali.

 

Akizungumza katika ziara ya kutembelea miradi ya nyumba za makazi na biashara za jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa kamati hiyo Dakta Hadji Mponda amesema shirika limepata faida ya shilingi bilioni 31.5 mwaka jana na wamelipa kodi kwa serikali.

 

Hata hivyo Dakta Mponda amesema wameiagiza bodi ya shirika hilo kuishauri serikali kutengeneza sera mpya ya nyumba inayoendana na ukuaji wa sekta hiyo pamoja na kupunguza bei za nyumba.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment